Wednesday, May 29, 2013

NI MARUFUKU CLOUDS FM KUPIGA NYIMBO ZA NGWEIR ZILIZO CHINI YA BONGO REC MAJANI


Kufuatia kifo cha msanii mangweir kilichotokea huko Africa ya kusini kwa kile kinachodaiwa na wadau kuwa ni kutokana na kuzidisha ulaji wa unga uliompelekea kupoteza maisha huku bongo nako yameibuka mapya hasa kutokana na sakata lililokuwa llinaendelea kati ya wasanii na menejiment ya clouds fm ya hapa jijini.

Kama mtakumbuka redio hii ilikuwa na mtafaruku mkubwa na msanii ambaye kwa sasa ni muheshimiwa mbunge joseph mbiliny  Mr 11 ama sugu kwa kile kilichodaiwa ni kunyanganywa mradi wake na kudhulumiwa haki yake,na hivi karibuni tukasikia sakata la mwanadada judith wambura maarufu kama Lady Jay Dee commando au Ana conda kama anavyojiita akidai kukandamizwa na redio hiyo jambo lilifanya kufikishana mahakamani.

Sakata hilo limechukua sura mpya mara baada ya kupokea taarifa za msiba wa ngweir kwani wasanii walioshirikiana na mangweir kwenye nyimbo zao na ma produser waliotengeneza nyimbo za ngwer kwa pamoja wamegoma nyimbo hizo zisipigwe na clouds fm kwa kile walichodai kuwa jamaa ni wanafki.

Photo: Tembelea DJCHOKAblog kwa habari zaidi..
Huu ndio ujumbe wa p funk kwa clouds fm
Akipiga stori na waandishi wa habari P funky Majani wa bongo recod amesema yeye binafsi ana amini kuwa clouds imechangia kifo cha msanii huyo kwani ilimkandamiza sana na ndio sababu ya yeye kupoteza dira na kujikuta akitumia unga kama kupoteza mawazo.

Majani amesema nyimbo kama mikasi na nyingine nyingi alizozitengeneza yeye na zile anazozimiliki yeye ni marufuku kupigwa na redio hiyo kwani walishamwaga msanii huyo kitambo hivyo wasijifanye kujipendekeza sasa hivi baada ya kifo chake wakati wao walichangia msanii huyo kushuka na kuwa na maisha mabovu.

Pia majani amewaomba watanzani wawe na mshikamano kwani clouds inaharibu soko la muziki wetu na kufanya wasanii wayumbe hivyo amesema atatowa barua rasmi muda mfupi ujao kusitisha upigwaji wanyimbo zake katika redio hiyo na kuongeza huu ni muda wa mapambano.
 
Wengine ni ludigo ambaye amefanya kazi nyingi sana na wasanii wa bongo fleva akiwemo marehemu naye hakupishana na Majani kwani ameomba haki zake na za marehemu zilindwe kwani nyimbo hizo hata zikipigwa kwa sasa hazitasaidia na wala hazitampa marehemu faida,


Akipiga stori na blog hii mdau kutoka marekani amesema,Nyimbo hizi zilitzkiwa zipigwe wakati mshikaji yupo hai leo mnazipiga na kuzipa kipaumbele ili zimsaidie nani wacheni unafki wenu hamuwasaidii wakiwa hai ili wale matunda badala yake mnawakandamiza na kuinua wasanii wenu wasiojiweza mithili ya bazoka zinavyokwisha utamu alafu wasanii wa kweli mnawafukia wakifa mnajifanya kupiga nyimbo zao hatutaki alisema abduu mdau wa mziki aishie marekani

Ama kwa hakika bado mambo ni magumu na ninaimani yataibuka mengi kutokana na sakata la wasanii na chombo hicho cha habari nitawaletea mengi yatakayojiri katika msiba huu wa ndugu yetu kipenzi Albert Mangweha.

1 comment:

  1. I entirely concur with Majani

    ReplyDelete