Wednesday, May 08, 2013

BAADA YA KUJIUZA KWA MIAKA KADHAA, AUNT LULU WA BONGO AAMUA KUBADIILI UPEPO WA MAISHA

Siku chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kunaswa kwenye mtego wa kujiuza, sasa ameamua kubadilisha mfumo wa maisha aliyokuwa akiishi zamani na kuwa na mwingine mpya.

Akiongea  na  mwandishi  wa  habari  hii, Aunty Lulu alifunguka kuwa kwa sasa ameamua kubadilika kwani kama ni starehe amefanya sana pamoja na uchafu mwingi ila kutokana na mtego wa kujiuza kumnasa na ushauri aliopewa na familia yake, amebadilika na sasa amegeukia kwenye ujasiriamali.
 
“Yaani kutokana na mtego wa kujiuza nimeamua kubadilika kwa sababu jamii ilinichukulia tofauti sana hivyo nikaamua kufanyia kazi ushauri wa familia yangu niliokuwa nikipewa kila siku lakini nikawa naukataa.


Kwa sasa nafanya ujasiriamali na ninafurahia maisha haya kuliko yale niliyokuwa nikiishi zamani.

Aunty Lulu kwa sasa anamiliki duka la vipodozi na ni wakala wa kutoa na kuweka fedha kwa kupitia mitandao ya simu za mkononi maeneo ya Kinondoni Kanisani, Dar ambapo ndipo anashinda kwa sasa na kwa mujibu wake  ameachana kabisa na kujiachia kwenye sehemu za starehe na kufanya mambo yasiyotakiwa katika jamii.

No comments:

Post a Comment