Sunday, May 26, 2013

UAMSHO YAKUSANYA SAINI 60,000 ZA KUHOJI MUUNGANO WA TANZANIA...

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kislamu (JUMIKI) imekusanya zaidi ya majina elfu 60 na saini zao kwa ajili ya kudai kura ya maoni ya kukataa au kuukubali Muungano.

Akitoa taarifa ya Jumuiya hiyo kwa wandishi wa habari huko hoteli ya Mazson, Naibu Amir wa Uamsho, Sheikh Haji Ali amesema jumuiya hiyo inaamini Muungano uliopo umefanywa bila ya ridhaa ya wananchi.

Amesema hivi sasa umefika wakati kwa Wanzanzibari kudai kura ya maoni na mustakabali wa Zanzibar.

Aidha, Sheikh Ali amesema Uamsho itaendelea na shughuli zake za kuelimisha, kutetea na kudai Zanzibar yenye 

mamlaka kamili Kitaifa na Kimataifa bila ya kuvunja  sheria na taratibu za nchi.

Amesema baadhi ya viongozi kwa utashi wao wa kisiasa wamejaribu kuzuia mihadhara ya Jumuiya hiyo, lakini hatua hiyo imefanyika nje ya sheria kwa vile Jumuiya hiyo imesajiliwa kisheria.

Wakati huo huo, jumuiya hiyo imekanusha taarifa zainazoenezwa na vyombo vya habari na wanasiasa kuihusha na vurugu na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwemo uchomaji wa makanisa, maskani na mauaji.

---
via ZanzibarIslamicNews blog

No comments:

Post a Comment