Saturday, May 18, 2013

WASANII WA BONGO MOVIE NENDENI MKASOME MSIDANGANYWE NA USTAR UCHWARA

Msanii wa filamu nchini tanzania mwenye majina kibao huku akizidi kukimbiza katika filamu za hisia kali hadi kubatizwa jina la baba wa hisia,,haji adam dach au baba adam ameongea na the super stars tz kwa mara ya kwanza kutokea bagamoyo anakosomea maswala mazima ya sanaa 

Akipiga story na sisi mjini bagamoyo katika chuo cha sanaa haji ameseme kuwa sana ina mambo mengi na inahitaji elimu kubwa sana na juhudi ili kufikia mafanikio kama wenzetu,msanii huyo mwenye mashabiki wengi ameeleza kuwa sanaa bila elimu ni kazi bure kwani upo uwezekano mkubwa sana tasinia hii ya filamu kuwa kubwa sana hapa nchini na kuleta wawekezaji wakubwa kutoka hollwood,india,filiphin na mataifa mengine makubwa kuja kuwekeza hapa katika filamu sasa wale hawataki longo longo wanafuata kipaji kisha  elimu,,na hii itakusaidia kuvuka mipaka na kuwa wa kimataifa zaidi

Haji ameyaongea hayo na kueleza huku akionyesha dhahiri kufurahi maisha ya kielimu...Kwa sasa

nimejipanga vyema nashukuru mungu nipo katika hatua za mwisho kumaliza chuo hivyo nategemea kuitumia elimu niliyoipata chuoni na hata kwa marafiki kutoka nnje ya nchi kama finland na nchi nyingine ambao hufika chuo cha bagamoyo kwa ajili ya kubadilishana mawazo hivyo nimejifunza mengi sana alisema haji nakuongeza kuwa ,,Nawashauri wasanii wasome kama kweli wanadhamira ya kweli katika kuinua sanaa yetu ya tanzania ,wasanii wanatakiwa watambue kuwa elimu haina ustar na tusidanganywe na ustar wetu uchwara na badala yake kila msanii apatapo uwezo kidogo ni vyema kupata elimu ili kujiweka tayari na harakati za kulivaa soko la kimataifa.

Baba haji ameieleza thesuper stars tz kuwa kwasasa hana kitakachokuwa kikimsumbua hivyo amerudi katika game na ana vitu vingi na kuahidi kufanya makubwa kabla hajaelekea nchini finland,danmark,na mwisho atamalizia ziara yake nchini marekani ambapo atajifunza namna kuandaa eneo yaani location za filamu ili kuondokana na matatizo ya kuomba nyumba halisi,Nimejifunza mengi sana na nimepata bahati nitasafiri nchi kama tatu nilizoalikwa na marafiki zangu kutembelea vyuo vyao na kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo uongozaji wa filamu kiukweli nashukuru sana kwani bagamoyo imenipa mwanga halisi wa maisha ya filamu alisema haji kwa sasa ni raisi wa chuo cha sanaa cha bagamoyo.

Haji ameomba serekali iangalie sanaa ya tanzania kwani inawakosesha mamilioni ya shilingi wasanii kwa uzembe wakutolifuatilia swala hili hivyo amesema anaimani serekali ni sikivu na italifanyia kazi swala la wasanii kwani wao kama wasanii wanchi hii wanataka sanaa ifike levo za mbali sana afrika kwani kwa uchache wa nguvu zao wameweza kuiteka afrika mashariki na sasa wanaelekea mashariki ya kati hivyo wanachoomba ni serekali kuwatambua kwa vitendo na si kwa maneno. alisema baba haji

No comments:

Post a Comment