Saturday, May 18, 2013

YANGA YAICHAPA SIMBA 2-0, VURUGU ZATOKEA UWANJANI REFA APIGWA


Shabiki wa Yanga ambaye jina lake halijapatikana alikatwa kidole baada ya jazba kati ya washabiki wa timu za Yanga na Simba zilizopelekea Mashabiki hao kuchapana makonde leo kabla ya mechi kuanza.Tukio hilo lilitokea katika eneo la Mwembe Yanga.

Timu ya Yanga imeonyesha ubingwa kwa kuichapa timu ya Simba mabao 2 kwa 0 huku vituko na vioja vingi vikijili uwanjana ikiwepo  kichapo  kwa  refa.. 

Listi ya wachezaji  wa timu zote mbili ilikuwa  ni kama ifuatavyo:
 
Simba SC : Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba na Haruna Chanongo. Sub: Abel Dhaira, Miraji Adam, Ramadhan Singano ‘Messi’, Felix Sunzu, Christopher Edward, Jonas Mkude na Hassan Mkude

Yanga FC : Ally Mustapha ‘Barthez’, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Athuman Idd ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima. Sub: Said Mohamed, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nurdin Bakar, Nizar Khalfan, Said Bahanuz na Jerry Tegete

Ndani ya dakika 8 za mwanzo  katika kipindi cha kwanza, vijana  wa Jangwani walifanikwa kumchapa  Simba SC bao 1. Bao hilo lilipachikwa  na Didier Kavumbagu

Baadaye Mshambuliaji Hamis Kiiza aliipatia Yanga bao la 2 dakika ya 63 baada ya piga nikupige katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam 


PAMOJA NA KUMCHINJA MYAMA KATIKA MECHI HIYO YA KUTIMIZA WAJIBU (YANGA WALISHATANGAZWA MABINGWA SIKU KADHAA ZILIZOPITA), YANGA PIA IMEKABIDHIWA KOMBE LAKE LA UBINGWA MBELE YA UMATI WA WATAZAMAJI 60,000 WALIOFURIKA UWANJANI HAPO. HII NI MARA YA 24 KWA YANGA KUIFUNGA SIMBA WAKATI SIMBA IMEWAFUNGA YANG MARA 19. ILA HADI SASA SIMBA INAONGOZA KWA KUIFUNGA YANGA KWA MABAO MENGI, IKIWA NI PAMOJA NA 6-0 NA MABAO 5-0 AMBAYO BADO YANGA HAWAJAJIBU MAPIGO.

No comments:

Post a Comment