Saturday, June 15, 2013

ANGALIA JINSI SHOW YA LADY JAY DE ILIVYOFURIKA WATU HADI WAKAANZA KUBEBANA PALE NYUMBAN LOUNGE

Mwanadada Judith Mbibo aka Lady Jaydee usiku wa kuamkia Jumamosi ya June 15 amefanikiwa kuweka historia kwenye muziki wa Tanzania kwa kulijaza eneo zima la Nyumbani Lounge alipokuwa akifanya show yake ya kuadhimisha miaka 13 tangu aanze muziki. 
 
Hii imedhihirisha kuwa majina anayojiita mwanadada huyu ni ya halali kabisa na yanamfaa kwani tafauti na watu walivyodhan palijaa watu hadi wakaanza kubebana ama kwa hakika huyu ni komando,anaconda hebu anagalia picha mdau utakubaliana na mimi
Hivi ndivyo hali ilivyo ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo leo hii kuna bonge moja la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii wanamuziki mbali mbali wamepanda jukwaani akiwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
 Wadau mbali mbali wa muziki hapa nchini wapo ndani ya ukumbi huu kusuhudia show hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki.
 Ndani ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama ilimradi tumsapoti Dada yetu."
 Getini mambo yako namna hii.

 Foleni bado ni ndefu na watu bado wanazidi kuingia ukumbini hapa hivi sasa.

DSC_4275

Katika show hiyo, Lady Jaydee amesindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Juma Nature, Sugu, Profesa Jay, Wakazi, Grace Matata na wengine. Pia Jaydee ameitumia siku hiyo kuzindua albam yake mpya, Nothing But The Truth na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Hizi ni picha za show hiyo.

DSC_4279DSC_4285

DSC_4288


DSC_4291

DSC_4293


DSC_4299

DSC_4300


DSC_4301

DSC_4445DSC_4447

DSC_4449


DSC_4466

DSC_4261


DSC_4273

Picha  kwa  hisani  ya  Bongo5
 
VIDEO  YA  MAKAMUZI

9 comments:

 1. Ebana eeeeeeeeeeeee UMETISHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA DADA wapi mwanaFATUMA

  ReplyDelete
 2. ni noma dada unaweza penda sana ww

  ReplyDelete
 3. wapi MwanaFatuma na wafuz fm.. mamayo mashoga wale!!
  Big up kwa saaana Jide and the whole crewz

  ReplyDelete
 4. Lady Jide hongera sana kw uthubutu na ujasiri wako wa ktk kuitetea haki na maslahi yako toka ktk mikono ya majasusi wa kazi za wasanii.
  Lady Jidee kaza buti....!

  ReplyDelete
 5. Hiyo ndo Team Anaconda, Machoko Clouds a.k.a Wafu FM na Matako wao Mwana FA Wakajipange Upya

  ReplyDelete
 6. HONGERA SAAAAAAANNNNNAAAAAAA ME NILIENJOY HAD BASIIIIIIIIII

  ReplyDelete
 7. umetisha dada jide.......clouds was.......n...g......e sana na mwanafatuma wao

  ReplyDelete
 8. proud of u as a strong woman.keep moving and never ever back up on any challeng,if they want something tell them to come.

  ReplyDelete