Sunday, June 30, 2013

BEYONCE NA KIVAZI CHA KANGA, ILIYOTENGENEZWA NA MBUNIFU WA KITANZANIA

BEYONCE

Utajiskiaje kuona Beyonce akiwa amevaa vazi lililotengenezwa kwa kanga yenye maneno ya Kiswahili? ‘Wawili Ninyi Yawahusu….’ yanasomekana maandishi kwenye vazi alilolivaa mwanamuziki wa Marekani, Beyonce Knowles. Vazi hili alilolivaa Beyonce kwenye moja ya show zake za tour ya Mrs Carter, limetengenezwa na mwanamitindo wa Tanzania aishie jijini London Uingereza, Christine Mhando mwenye brand ya Chichia London. Chichia London ndio brand iliyo maarufu sana nchini Uingereza kwa kutengeneza nguo za Kitanzania kwa kutumia Kanga na material mengine Kiafrika. Kwa Picha zaidi

No comments:

Post a Comment