Monday, June 03, 2013

BIG BROTHER: MSHIRIKI WA TANZANIA APEWA KAZI YA KUTEMBELEA MIGUU NA MIKONO KWA MUDA WA SIKU TANO


SHINDANO la Big Brother Afrika limeendelea kwa washiriki wawili kutolewa katika wiki ya kwanza ya mchezo huo ambao unashirikisha washiriki wapatao 28 kutoka nchi 14 barani Afrika.

 Jumatatu iliyopita washiriki walipata nafasi ya kutoa mapendekezo yao ya kuchagua washiriki ambao wanaona wanafaa kuingia katika Danger Zone ambapo watano kati yao ndio waliotajwa mara nyingi zaidi na washiriki wenzao hivyo kuingia huko. 

Washiriki waliongia katika Danger Zone walikuwa ni Betty wa Ethiopia, Selly wa Ghana, Denzel wa Uganda, Natasha wa Malawi na Huddah wa Kenya ambapowatazamaji walitakiwa kumpigia kura mshiriki ambaye wanaona anafaa kubakia ndani ya jumba hilo. 

Katika kura zilizopigwa na watazamani kutoka nchi 14, Betty ndio alipata kura nyingi zaidi baada ya kupata kura 5, akifuatiwa na Selly na Natasha waliopata kura tatu kila mmoja huku Denzel na Huddah wao wakiambulia kura mbili hivyo kumaanisha kwamba safari yao katika kugombea dola 300,000 kuishia hapo.
 Baada ya kutolewa katika jumba hilo IK mtangazaji wa kipindi hicho aliwapa nafasi washiriki hao kulipa kisasi kwa kuchagua mshiriki mmoja ambaye hupewa kazi ambayo hutakiwa kuifanya kwa muda atakaopangiwa.
 
Wa kwanza alikuwa Denzel ambaye alitakiwa kuchagua mshiriki ambaye atatakiwa kila akitoka nje kupunga hewa kwenye jumba hilo awe anatembea kwa miguu na mikono kwa muda wa siku tano na kijana huyo hakusita kumchagua Nando mshiriki wa Tanzania kufanya kazi hiyo. 
Aliyefuata alikuwa na Huddah ambaye yeye aliambia achague mshiriki ambaye atakuwa akitandika vitanda vyote katika jumba hilo kwa muda wa siku mbili na mwanadada huyo mrembo kutoka Kenya alimtaja mwanadada mwenzake Dillish kutoka Namibia kufanya zoezi hilo. 
Shindani hilo linaendela tena leo ambapo washiriki watatakiwa tena kupendekeza majina ya washiriki ambao wataingia katika Danger Zone kwa ajili ya kupigiwa na mashabiki ambapo atakayepata kura chache ataliacha Jumba hilo Jumapili ijayo.
pro24

No comments:

Post a Comment