Thursday, June 06, 2013

HII NDIO HALI ILIVYO KWENYE MSIBA WA MUME WA KHADIJA KOPA.....VILIO VYATAWALA KILA MAHALA..!!

SIMANZI, vilio na majonzi vilitawala nyumbani kwa Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, Tandale jijini Dar. Marehemu Jaffari ambaye alikuwa ni mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

Marehemu Jaffari alikuwa Diwani wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati mama yake mzazi ni Mwenyekiti wa UWT Tandale. Mungu ailaze roho ya marehemu Jaffari Ally mahali pema peponi.
No comments:

Post a Comment