Wednesday, June 05, 2013

HIVI NDIVYO LEADERS CLUB INAVYOANDIKA HISTORIA MPYA KUFUATIA KIFO CHA NGWEA

NIKIWASILI katika viwanja hivi vya Leaders Clabu dakika tano zilizopita nakutana na umati wa watu katika maeneo haya, shuguli mbalimbali za maandalizi ya mahali itakapowekwa jeneza la Mwili wa Albert Mangwea zikiendelea.
Kuna makundi mbalimbali ya vijana wakijadili hoja mbalimbali, zinazohusu tasinia ya muziki wa kizazi kipya pamoja na tasnia ya sanaa ya filamu nchini.
Katika mazungumzo ya vijana hao hoja na kumbukumbu zinawarudisha katika msiba wa aliyekuwa msanii wa filamu Steven Kanumba,aliyefariki dunia April 7 mwaka jana na kuagwa na umati mkubwa katika viwanja hivyo.

Leo hii tasnia ya muziki wa kizazi kipya pia ina andika historia nyingine katika viwanja hivyo kufuatia tukio la kuangwa kwa msanii kipenzi cha wadau wa muziki, msanii pekee aliyewahi kuhamasisha vijana wa kitanzania kujali mahali pakulala, yaani Getto,Mangwea aliamshia hisia za vijana baada ya kutoa kibao chake cha Getto Langu.
Katika Kibao hicho Mangwea alitumia kipaji chake kufundisha vijana jinsi ya kuishi mahali pazuri jinsi ya kuandaa mageto yako, lakini pia ikawa ni changamoto kwa vijana waliofikia umri wa kuingia katika mahusiano ya mapenzi yenye malengo ya kujenga familia kwa maana ya kufikia uamuzi wa kuona.
Katika kibao hicho Mangwea alikumbusha vijana ni jinsi gani watoto wakike (wasichana) wanavyovutiwa na vijana wasafi watanashati kuanzi mavazi yao hadi magetoni kwao, kiasi cha kubadilisha hata wale waliokuwa wachafu na kuwa wasafii

No comments:

Post a Comment