Tuesday, June 11, 2013

"KAMA NINGEKUWA RUGE NINGEMPIGIA MAGOTI LADY JAYDEE NA KUMUOMBA MSAMAHA"....SEBO WA MAGIC FM


Katika kipindi cha Sun Downer cha Magic FM, mtangazaji huyo amesema kwamba shangwe zilizolipuka mara baada ya Jaydee kutajwa kuwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya msanii bora wa kike katika  tuzo za KTMA, ni ishara ya mwanadada huyo kukubalika katika  jamii. 

Mtangazaji huyo amesema kwamba Jaydee ni mwanamke mwenye uthubutu katika  harakati za kuyasaka maisha na kwamba yeyote mwenye nia ya kukwamisha jitihada zake aibu na iwe juu yake. 

Ameongeza kuwa kukubalika kwa mwanadada huyu pia kulidhihirika pale  watazamaji katika tukio hilo walipomshinikiza Meneja wa msanii huyo (Gadna) kutaja kiingilio na tarehe ya maadhimisho ya miaka 13 ya Jaydee katika  uga wa muziki. 

Hivyo, Sebo anaona ni vyema Ruge akajishusha na kumaliza tofauti zake dhidi ya Jaydee

2 comments:

  1. hiyo ngumu sana, jay dee ndo wa kuomba msamaha

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwa nn jide aombe msamaha!?

      Delete