Monday, June 17, 2013

KAMPUNI YA RJ COMPANY YASHUKURU MASHABIKI...RAY ASEMA BILA MASHABIKI HAKUNA RAY

Ofisi ya Rj Inavyoonekana kwa Nnje
Kampuni bora ya utengezaji filamu tanzania iliyochukua tena tuzo kwa mara nyingine na kuifanya kuwa kampuni namba moja  iliyo na tuzo nyingi tanzania ijulikanayo kwa jina la Rj Kampani limited ya jiji dar juzi imejinyakulia tena tuzo nyingine ya kuwa kamuni bora ya utengeza wa filamu tanzania huku mmiliki wa kampuni hiyo bwana Vicent kigosi akijinyakulia tuzo ya Muongozaji bora wa filamu tanzania.

Ray akiwa ofisini kwake
Mwandishi wa thesuperstarstz leo alibahatika kutembelea ofisi hizo zilizopo maeneo ya sinza na kuongea na msanii huyo nguli ambaye pamoja na kushukuru amesema kwanza anawashukuru mashabiki wote waliofanikisha yeye kupata tuzo hizo kwani anaamini bila mashabiki yeye asingekuwa Ray na wala asingepata tuzo alisema msanii huyo.

Pia msanii huyo ameipongeza kampuni iliyotoa tuzo  hizo Steps ambao pia ni wasambazaji wa kazi za filamu tanzania,Ray amesema kuwa kampuni hiyo imethubutu kwani ni kipindi sasa kwa hapa nchini wasanii wamekaa bila kuonyeshwa kuwa wao ni wathamani hata kwakuwapongeza Kusema kweli bado tunahitaji watu watakao jitolea na kuleta changamoto kama steps kwani msanii kumpa tuzo ni  kumfanya ajue kuwa anatambulika hivyo kuifanya jamii kuzidi kukubali kazi zetu alisema ray

Hizi ndizo tuzo Rj ilizochukuwa
Kwa upande wa mkurugenzi mwenzake blandina chagula Johari amesema kwake yeye ni fahari kubwa kampuni yake kupata tuzo hiyo ya kampuni bora kwani kila mwaka huwa wanachukua na kuahidi kufanya mazuri zaidi katika kazi ili kuwafanya mashabiki wazidi kutuunga mkono alisema Johari

Akizungumza kwa upande wa soundman bora wa mwaka ambaye pia ni mfanyakazi wa kampuni hiyo bwana Saidi Baraghash amesema anafurahi kuona tuzo hiyo imekuja Rj na kuahidi kujituma sana ili kuleta tuzo nyingi zaidi

Kampuni ya Rj kwasasa inajiandaa kwaajili ya kazi yake mpya itakayoiwakilisha tanzania kimataifa na kuifanya kujitangaza zaidi alisema ray

No comments:

Post a Comment