Sunday, June 02, 2013

KIFO CHA NGWEA BADO NI UTATA....PICHA YAKE AKIWA MOCHWARI IMEIBUA MASWALI MENGI YANAYOHITAJI UCHUNGUZI WA KINA


Kifo cha mwanamuziki wa Tanzania, Albert Mangwea kilichoripotiwa hivi majuzi, kinazidi kuacha maswali mengi kadiri siku zinavyozidi kusogea.

Wapo baadhi ya watu ambao wametoa maoni ya kutilia shaka maelezo na sababu za awali za kifo hicho, hali wakitumai kuwa mtu aliyekuwa naye karibu ambaye anaelezwa kuwa hai bado hospitalini, mwanamuziki M2P huenda akawa mtu muhimu wa kutoa maelezo ya kusaidia kuelewa hasa kilichotokea.

Picha ya marehemu Mangwea akiwa katika chumba cha maiti, ambayo si vyema kuiweka hadharani moja kwa moja (bofya hapa kuitizama), inaonesha sura yake na shuka vikiwa vimezungukwa na utando mwekundu kama damu na hivyo kuacha shaka zaidi ya majibu endapo ni kuzidiwa kwa dawa za kulevya kulikotajwa kuwa sababu ya kifo chake, ama kuna la zaidi.

Majibu zaidi yatatoka ikiwa uchunguzi wa kina utafanyika, vinginevyo itabakia kuwa sababu halisi ya kifo cha marehemu ni siri aliyoondoka nayo.


Barua ya Mchango wa maandalizi ya mazishi

Picture

No comments:

Post a Comment