Sunday, June 30, 2013

LULU AFANYA INTERVIEW NA ZAMARADI KWA MARA YA KWANZA TANGU ATOKE JELA

Lulu  akiwa na Zamaradi
Hottest actress in Swahili movie industry Elizabeth Michael(Lulu) amefanya interview yake rasmi ya kwanza na Zamaradi Mketema wa Clouds Tv ikiwa ni takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa sasa tangu muigizaji huyo alipopata misukosuko ya kupelekwa segerea na baadaye kutoka kwa dhamana. 

Katika interview hiyo inayotegemewa kurushwa hivi karibuni inaelekea muigizaji huyo atazungumzia maisha yake ya  segerea na mipango yake ya kuliendeleza libeneke la filamu kama kawaida na mambo mengineyo

"kwa zaidi ya mwaka na nusu sasa!!! hii ni interview yangu ya kwanza baada ya kipindi chote hicho....thanks Zamaradi..." aliandika Lulu katika mtandao mmoja wa kijamii.

 Hata hivyo licha ya muigizaji huyo kukaa zaidi ya mwaka na miezi kadhaa sasa bila interview yoyote au kuigiza filamu mpya lakini bado mara kwa mara habari na picha zake zimekuwa zikipamba blogs na magazeti. huku watayarishaji wengi wakitaka kufanya nae kazi.


No comments:

Post a Comment