Friday, June 28, 2013

MAMA KANUMBA APANGA KUZIFANYIA SHEREHE TUZO ZA MWANAYE...!!


MAMA wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka kuwa yupo katika maandalizi ya sherehe (mnuso) ya tuzo za mwanaye ambazo amezipata kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu afariki dunia.
Akichonga na Nasi juzikati, mama huyo alisema tangu Kanumba afariki dunia amepata tuzo zipatazo tano hali inayompa faraja na wakati mwingine kuhisi kama mwanaye bado yupo hai.
 “Niko kwenye maandalizi ya kufanya sherehe ya tuzo za mwanangu Kanumba kwani nimepewa tuzo zake zipatazo tano ambazo zimekuwa faraja sana kwangu na kujiona kama niko naye, kutokana na heshima ambayo anapewa najiandaa muda wowote nitazifanyia pati tuzo hizo,” alisema mama Kanumba.

No comments:

Post a Comment