Sunday, June 16, 2013

MASTAR WA BONGO MOVIES WAMTOSA BABA HAJI KATIKA MAHAFALI YA CHUO

Msanii wa filamu tanzania ambaye ameamua kuwekeza katiaka kusomea filam huko chuo bagamoyo katika chuo cha sanaa Haji Adam Dach amemafanya mahafali yake na kumzungumza na thesuperstarstz.

Akizungumza na mwandishi wetu baba haji amesema kuwa kwanza anayofuraha kutimiza malengo yake ambayo alikuwa anayaota kila siku na pia anaamini kuwa sasa atafanya kila linalowezekana ili kuleta mabadiliko ya sanaa nchini tanzania.

 Msanii huyo ambaye ni raisi wa chuo hicho ameelezea furaha yake na kusema Kaka  kwanza namshukuru mungu sana  kumaliza japo masomo ni magumu ila kwa uwezo wa mungu nahitimu,Kuna masomo mengi yanayofundishwa hapa, mimi nimesomea somo langu kuu Acting, Directing, Management, Script writting, film criticism, Information Communication Technology, Research, Community theatre, Lighting setup, Production, Scenery, Media & sound design and Theatre in education. Masomo haya yote nimeyasoma katika kipindi chote cha miaka mitatu ya Chuoni, hali ilikuwa ngumu na masomo ni magumu lakini maji ukiyavulia nguo ni vema kuyaoga. alisema baba haji ambaye ni baba wawatoto wawili
Muda wote haji alionekana mwenye furaha japo furaha yake ilianza kupotea baada yakona muda una kwenda na wasanii wenzie ambao kwake ni kama ndugu wakiwa wamemtosa na kutokufika kabisa katika sherehe hizo zilizofanyika katika maeneo hayo ya chuo Kaka unajua siamini kabisa kaka yaani hadi sasa naona ndugu zangu wamenitenga na hakuna dalili za kufika kwao maana nimepiga simu nyingi zinaita bila majibu huku nyingine zikiwa zimezimwa kabisa

Mwandishi wa thesuperstarstz alibahatika kukutana na msanii Single mtambalike au Rich Rich na kuongea nae ambae alisema kuwa hata mimi sitaki kuamini kama mastar wameamua kumtosa mwenzao kwani wote wanajua na ilibidi jamba kama hili tuungane kwani haji ameonyesha mfano kwa kwenda kuwekeza katika elimu sasa inanishangaza sijui ni wivu au ni roho mbaya hata sijui mimi imeniuma sana kaka alisema Rich

Wasanii waliowasili katika mahafali hayo ni pamoja na Rich Rich,Natasha na Monalisa jambo lililofanya baathi ya watu wa chuoni hapo kupigwa na butwaa kwani wanachuo walijipanga kukutana na mastar ambao iliaminika wangeenda kumsapoti super star mwenzao ambaye ametumikia chuoni hapo kwa miaka mitatu sasa.

Baadhi ya wanachuo waliongea na thesuperstarstz nakuonyesha kutopendezwa na tukio lile na kusema hawajamtendea haki ndugu yao ambae amekaa nao katika gemu kwa miaka kumi na mbili sasa lakini wameshindwa kumsapoti,walisema wanachuo hao na kuponda ustaa wa tanzania.

No comments:

Post a Comment