Friday, June 07, 2013

MSANII MRISHO MPOTO AELEZA KIUNDANI KWANINI ANATAKA KUGOMBEA UBUNGE.

                                                           Mrisho Mpoto.

Hii ni mara ya pili baada Jumatatu ile ya february 4 2013 msanii Mrisho Mpoto alipoongea kwa mara ya kwanza kupitia AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kwamba mwaka 2015 ataingia kugombea Ubunge kwenye jimbo lolote Tanzania ambalo mbunge wake analegalega.

Baada ya taarifa yake kusikika alipokea simu 80 zikiwemo 12 za wanasiasa pamoja na sm 400 kutoka kwa watu mbalimbali ambao wamempongeza na wengine wakimuuliza maswali huku wabunge wakiongea nae kuhusu kujiunga nao

Leo tumekutana nae na kumuuliza machache kuhusu msimamo wake huo na kusema ana nia thabiti na lazima atimize kwa uwezo wa mungu kwani watu hawasikii wamejifanya mungu mtu sasa ni lazima sauti hii ya wanyonge ikalichome bunge.

Namkariri akisema “ni wazo ambalo limetoka kwa wananchi wenyewe wakisema nadhani tumekosea kupeleka mwakilishi, nadhani mwakilishi wetu ni wewe kwa hiyo ile demand ya wananchi imekua kubwa, nikasema hapana sasa lazima niende mwenyewe maana watu hawatusikilizi wamekuwa ni miungu watu wanataka kuabudiwa kila siku huku tunaowaabudu hatupati kitu sasa ni lazima niende kuwaamsha na kuwa kumbusha kuwa sasa wanyonge wote tupo macho alisema mpoto

Amesema “nimekua mwakilishi wa wananchi kwa muda mrefu kupitia nyimbo zangu lakini watu hawataki kusikia wala kubadilika, tunapozungumzia maisha tunazungumzia madirisha manne, kuna dirisha la  kwanza ambalo wananchi wanajua wewe hujui, la pili mwananchi hajui kama wewe hujui kuwa yeye anajua, la tatu mwananchi hajui na wewe hujui, la nne wewe unajua mwananchi anajua kwa hiyo dirisha hili wawakilishi wetu wamekua wakitumia vibaya sana wanafikiri wananchi hawajui wao ndio wanajua, ile dhana ya kuona wananchi hawajui ila wao ndio wanajua tunataka tukaionyeshe, tumezungumza sana”

“Hebu angalia mfano mzuri wa pale Mtwara, leo mpaka watu wanakufa mtu anasema siwezi kwenda kusaidia kule kwa sababu mimi si mbunge wa jimbo hilo, jimbo gani? wewe ni mbunge wa wananchi, unapokua mbunge ni mbunge wa Watanzania wote, watu hawataki kushughulika nao mpaka viongozi wanakuja kutoka huko ndio wanakwenda kule kuzungumza, haya mambo kama yanaweza kuzungumzwa yasingetokea? alafu unasema amekufa mtu mmoja tu watu wawili? ile pia ni roho, ile pia ni damu, tumeshindwa kusikilizwa hapa tutasikilizwa tukiwa kule kule ndani ” – Mpoto

Mwanahabari wetu alipomuuliza kuhusu chama mpoto alisema kwasasa ni  mapema sana kwani yeye haingii bungeni kutafuta chama bali maslai ya wananchi japo atakapokuwa tayari ataweka wazi nichama gani atakachoingia nacho bungeni

No comments:

Post a Comment