Sunday, June 30, 2013

MTOTO WA KIKE WA MANDELA AWAJIA JUU WAANDISHI WA HABARI WALIOPIGA KAMBI NJE YA HOSPITAL ALIYOLAZWA MANDELA

Mtoto wa kike wa Mpiganiaji Uhuru wa South Africa Nelson
 Mandela anaeenda kwa Jina la Makanziwe
Mandela,Juzi aliongea kwa ukali na kutoa tamko juu ya waandishi
 wa habari waliopiga kambi
nje ya hospital ambayo Baba yake kwa sasa amelazwa
akipigania maisha yake kutokana na
matatizo ya mapafu.....


Hali hiyo imekuja baada ya vituo vya habari kuweka kambi
 nje kwenye hospital hiyo iliyopo Pretoria....
Makanziwe akiongea kwenye simu kumjuza mwandishi wa habari
wa Ikulu kuhusu Hali ya mzee mandela
aliongea hivi ''Tunashukuru Mungu baba kwa sasa hali inaridhisha,
ni mtu mzima sana lakini Mungu anazidi
kutupigania na familia tunaamini atarudia hali yake kama
zamani na kujongea na sisi nyumbani....

Akizidi kuongea,ndipo alipofunguka juu ya waandishi wa habari
''Nachukizwa na kitendo hiki cha hawa
waandishi wa habari kabisa wanadiliki kuweka kambi nje ya
hospital kuripoti hali ya baba yangu,kusema kweli
sijapendezwa au kwa kuwa sisi ni waafrika ndio atupaswi kueshimiwa
 tunapoitaji undani wetu,nimechukizwa sana
yani wapo nje kana kwamba wanasubiri kitoke kitu wawe
 wa kwanza kuripoti......
Alizidi kusema ''Tunahitaji undani wetu kukiwa na jambo lolote
 familia itawajuza naomba heshima itumike na
busara kwajili ya mzee wetu,sidhani kama angekuwa yupo katika
hali nzuri angefurahia kuona kitu kama hiki''

Hayo ndiyo yaliyosemwa na Mtoto wa kike
mkubwa wa Nelson Mandela.....

No comments:

Post a Comment