Tuesday, June 25, 2013

OMMY DIMPOZ;SINA TATIZO NA MTU NAMINI HATA MAREHEMU NGWAIR ANAJUA KUWA SIKUMTUKANAAkizungumza na kipindi cha XXL mwanamzik
i Ommy Dimpoz alizungumzia tukio la yeye kulushiwa makopo
 stejini mjini Dodoma lakini zaidi alizungumzia kauli aliyoitowa wakati
 wa tuzo za Kili.......

"imeenezwa chuki kwamba mimi nimemtukana 
marehem Albert kitu ambacho sio kweli, nimejaribu 
kukielezea kwenye media mbali mbali kuwa si kweli, wametumia kauli yangu
 niliyoongea kupitia Killi siku ya Tanzania Music Awards wakati
 kitu nilichokiongea nitofauti na kitu kilichokuja 
kupandikizwa, lakini mi najua safari ya mziki ni ndefu, na
 mwenyezi mungu atajaalia tu haya mambo
 yatakwisha kwasababu hata yeye mwenyewe anajua
 sina kosa, sija mkosea mtu wala sina tatizo na mtu, nafanya tu
 maisha yangu ya mziki, lakini inapofikia time unajua mtu mwingine anaweza 
akaja tu na sababu zake binafsi kwa nia ya kukuvuta
 shati, lakini kama mungu amendika njia yako
 nyeupe basi itakuwa nyeupe tu, na hakuna njia iliyonyooka siku zote lazima
 inakua na vikwazo kidogo, kwa hiyo naamini hii ni 
mitihani tu itaisha kwasababu sina tatizo na mtu.
nachoamini binaadam tunakufa pengine roho pengine zinabaki zina hang, hata marehem mwenyewe naimani anajua kwamba sikumtukana...................
hii ni challenge tu  naichukulia kwangu, pengine
 ni mitihani kwasabau sijawahi kuipata na 
 ku experience katika maisha yangu ya mziki hiki ni kitu kikubwa
 nimekutana nacho kwa sasa, lakini naimani itakwisha."

hivyo ndivyo alivyofunguka Ommy Dimpoz

No comments:

Post a Comment