Sunday, June 02, 2013

REGINALD MENGI AMPONGEZA KIKWETE KWA KUUZA NCHI NA KUWAACHA WATANZANIA WAKIUMIA


 
WAKATI wawekezaji wakigeni wakizidi kunufaika huku watanzania wakiendelea kuishi katika lindi la umaskini,Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Media Reginald Mengi ameipongeza Serikiali ya Rais Jayaka Kikwete kwa hatua ya kuuza nchi kwa wawekezaji hao.
 
Pongezi za Mengi kwa Serikali ya Rais Kikwete imekuwa na tafsiri tofauti kutokana na jinsi ambavyo wawekezaji hao wananufaika kupitia migongo ya watanzania maskini na rasilimali zao, huku Rais Kikwete na Serikali yake ikiendelea kulifumbia macho suala hilo.
 
Mengi ambaye ni miongoni mwa watanzania wachache wanaotumia sehemu ya mali zao kuwasaidia watanzania wenye maisha magumu hususan walemavu wa viungo na ngozi, alitoa pongezi hizo kupitia akaunti yake ya Twitter.
 
"Hongera Tz kwa kuwa labda nchi ya kwanza duniani kubinafsisha mashirika ya umma na kunufaisha wawekezaji wageni badala ya wananchi"alitweets Mengi katika akaunti yake.
 
Kauli hiyo ya mengi pia imekuja ikiwa ni wiki moja tu tangu wananchi wa Mtwara wafanye vurugu kubwa zilizosababisha vifo vya watu wawili na kufanya uharibufu mkubwa wa mali.
 
Vurugu hizo za wanamtwara zilikuwa na lengo la kupinga hatua ya Serikali ya Rais Kikwete kusafirisha Gesi kutoka mkoani humo hadi jijini Dar es Salaam na hatimaye kufika Mkoani Pwani hasa katika Wilaya ya Bagamoyo mahali alipozaliwa Rais huyo. 

Kauli ya Mengi pia imekuja katika kipindi ambacho Tanzania inatarajia kupokea ugeni mkubwa katika historia ya nchi hii. Rais wa Marekani Barack Obama anatarajia kutembelea Tanzania mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu, akiwa na msafara wa watu 700 wenye lengo la kuja kuwekeza Tanzania. 
 
Ziara hiyo ya Obama inakuja ikiwa ni miezi minne tangu Rais wa Jamhuri ya watu wa China Xi Jinping alipotembelea Tanzania kwa ziara kama hiyo ya Obama...

No comments:

Post a Comment