Monday, June 10, 2013

SITEGEMEI WANAUME NATAFUTA PESA ILI NIJENGE MAISHA YANGU...JACKLINE WOLPER

Hapa Jackline wolper akikaribiswa chakula na kusema kashiba
Msanii wa filamu nchini tanzania jackline masawe wolper amesema hategemei wanaume kama ambavyo marafiki zake na jamii walivyomkariri.

Jack ameeleza kuwa yeye si mwanamke tegemezi ndio maana ameweza kumiliki kampuni yake mwenyewe ya filamu na biashara kibao ndani na nnje ya mkoa huu wa dar,Mwanadada huyo aliyasema hayo huku akidai anashangazwa na habari kuwa mwaka huu hana mwanaume ndio maana haonekani akifanya fujo mjini,jambo amabalo yeye anaona ni kituko kwani badala ya watu kufikiria au kumshauri awe na majumba makampuni makubwa wao wanataka kumuona jack wa mashoping na mastarehe kitu ambacho mwanadada huyo anasema kwasasa hayupo tiyari kwani ameshakuwa na ana majukumu mbele yake.
Hapa akiwaza jinsi ya  kujibu maswali picha hizi ni ndani ya kampuni ya bwana ray na johari iliyopo sinza ni ndani ya RJ Company tulipomkuta msanii huyu
Akipiga stori na mwandishi wa thesuperstarstz  jack alisema hana haja ya kupigizana kelele nao wanaojifanya kumjua wakati hawamjui ki hivyo kwani ana amini katika hii dunia kila mmoja ameletwa kwa kazi maalumu na hawezi kumuingilia mtu,,,Nashangazwa na watu wanaojifanya kunijua kiundani wakati hawanijui kihivyo mimi ninamaisha yangu na sina muda wa wakupiga soga na watu wasiokuwa na la kufanya.
Hapa ni moja ya pozi la mwanadada huyu

Mwanadada huyo ambaye kwa sasa inasemekana ndio taa ya mabinti sokoni kwani amesema kwasasa yupo kwenye mipango ya kushusha bonge la mjengo na kuwataka mashabiki zake waendelee kumuunga mkono kama ilivyo sasa,Na kuhusu kazi Jack anasema anamshukuru mungu kwani kafanikiwa vizuri sana nakusema kiutani kuwa ukitaka kujua jack ninani nenda kwa wauza cd watakuambia
Hapa akitaka kuaga mara baada ya kumaliza kilichompeleka katika ofisi za Rj Company
Alipotakiwa kumtaja mpenzi wake wa sasa jack alisema nadhani kwa sasa sintokuwa tiyari tena kwani naogopa maisha haya kila nikipata  mtu wangu wajanja wanabeba na mimi kazi ya kugombea mabwana mwenzenu siwezi kabisa,,,ila kwa sasa nikimpata nitahakikisha hadi watu wakimjua basi tiyari kashakuwa mume wangu alisema jack mwanadada mpole na mwenye tabasamu kila akiongea.
 Thesuperstarstz inamtakia kila la kheri katika safari yake hiyo

3 comments:

  1. kaza buti mama achana nao

    ReplyDelete
  2. Mie nampenda sana huyu dada.....keep it up..usijali maneno ya watu....wee jua kazi yako...na pia usimuache mungu kwani ndio aliyekufikisha hata hapo ulipo

    ReplyDelete
  3. Unaweza kabisa,una kila kitu wolper

    ReplyDelete