Tuesday, June 11, 2013

TINO AFANYA MAAJABU CHINI YA TIMAMU EFFECT.. SINGLE ZERO NI AIBU


Director wa filamu yenyewe na pia amehusika kama mchezaji
Ile kampuni ya utengenezaji filamu iliyopo nchini tanzania Timamu Effect ya jijini Daresalam imedhihirisha kuwa Elimu waliyoipata toka South Africa kwa madiba na ile walioipata toka kwa mkufunzi Berry Braveman toka Hollwood na Dipesh toka Bollwood imefanya kazi na kuzaa matunda.

Hili limejidhihirisha wazi mara baada ya kufanya filamu ijulikanayo kama SINGLE ZERO ya Hissan Muya Tino iliyofanyika chini yao kuanzia picha sauti edting na Directing,filamu hiyo ya mapigano imefanywa katika ubora wa hali ya juu na kuifanya kuwa picha ya aina yake ukiiangalia.

Moja ya scean ambazo zililazimu watu wakashut katika shel hii maaana story na director alitaka hivyo
Mwandish wa habari hii alibahatika kuona baadhi ya vipande katika ofisi za Timamu Effect zilizopo maeneo ya mbezi sal sala Nchi ya Ahadi kama wenyewe wanavyoiita.

Kwa hakika picha ni nzuri na nina imani itafanya vizuri sana ukizingatia mafunzo tuliyoyapata huko south Afrika na hapa kwetu chini ya mtu mzima john liber yametusaidia sana kuifanya hii kazi iwe na ubora wa ki filamu kwani hata ukiangalia kwasasa tanzania bado tupo katika mfumo wa maigizi na si filamu ila kuwepo chini ya huyu mzungu john liber aliyeongoza filamu ya NERIA tunaamini tanzania itapiga hatua sana katika filamu alisema Jacksoni kabirigi ambaye ni Director wa filamu hiyo.

Moja ya Scean katika movie ya SINGLE ZERO
Nae cameraman wa fialmu hiyo Timoth au Tiko amesema kuwa sasa umefika wakati watanzania tuache kufanya maigizo badala yake tuanze kujifunza namna ya kufanya filamu kwani elimu ipo bure kwa mtu kama John liber ambae ameamua kutoka kwao marekani kuja kutupa elimu ya filamu alisema Tiko na kuongeza kuwa Liber ni muongozaji mkubwa sana ukiangalia filamu kama NERIA..YELLOW CARD ni filaamu zilizo na tuzo nyingi sana sasa mtu huyu yupo hapa na ndio anayetupeleka kusoma ila cha ajabu baadh ya wasanii waliitwa wakakataa kwakujifanya wanajua sana alisea kwa masikitiko sana cameramani huyu anayejua kazi yake.

Kwa upande wa tino ambaye ndiye mmiliki wa filamu hiyo alisema kwanza amejifunza mengi toka kwa muongozaji huyo mdogo lakini mwenye akili nyingi sana,pia amejifunza kuwa filamu ni gharama sana tofauti na hizi zetu tunazosema filamu yaani tunakaa katika masofa mwanzo mwisho gharama inakuwa ndogo sana ukilinganisha na hii filamu niliyofanya chini ya Timamu Effect Kwanza jamaa wanajua wanachokifanya pili wao wanafuata stori inavyotaka ndio wanasaka location na hata kama scen moja itabidi ipigwe nnje ya nchi basi lazima uwapeleke la sivyo hawakuelewi nadhani ukiiangalia vizuri hiyo promo utagundua hiyo sheli tuliifuata moshi kwa ajili ya scen hiyo tu na imeshutiwa siku mbili hadi director aliporidhika ndio tukaondoka alisema tino.

Cameraman wa Timamu Effect akiwa na mkufunzi wa Camera toka India Bwana Debesh
Tino aliendelea kusema kuwa kupitia kwa wahisani wao watamleta msanii mkubwa toka hollwood marekan kuja kufanya uzinduzi wa filamu hiyo na kuwapa changamoto zaidi za nini wafanye ili kukuza filamu za tanzania,Thesuperstarstz ilipotaka kujua ni msanii gani tino alisema ni mapema mno kumtaja ila akasema ikikamilika mipango basi kila kitu kitakuwa wazi

No comments:

Post a Comment