Monday, July 01, 2013

BRAZIL YATWAA UBINGWA KOMBE LA MABARA, YAIKANDAMIZA SPAIN 3-0 BILA HURUMA

  Ndiyo maana soka ni mchezo unaopendwa na watu wengi zaidi duniani kwa kuwa hauna matokeo yanayotabirika na Hispania wanaweza kuwa shahidi wa hilo katika mechi ya fainali ya Kombe la Mabara iliyomalizika punde.
Wenyeji Brazil wametawazwa kuwa mabingwa baada ya kuwafunga mabingwa wa dunia, Hispania kwa mabao 3-0.

Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Maraccana ilikuwa burudani tupu na Brazil walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 2 mfungaji akiwa Fred na dakika 44, Neymar akafunga bao la pili kwa shuti kali.Kipindi cha pili, dakika ya tatu, Fred tena akafunga bao la tatu ambalo lilionyesha kumaliza matumaini ya Hispania ambayo baadaye Sergio Ramos alikosa mkwaju wa penalti.

Baada ya hapo, wenyeji ambao walianza soka kwa kasi tokea kipindi cha kwanza, walionekana kuendelea kuwabana mabingwa hao wa Ulaya na dunia.

Mshambuliaji Neymar amepewa nyota wa mchezo mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Hispania waliendelea kujitahidi kupambana hata baada ya beki wake Pique kulambwa kadi nyekundu kutokana na kumkwatua Neymar akiwa anakwenda kumuona Casillas.

No comments:

Post a Comment