Saturday, July 27, 2013

HABARI KUHUSU ALLY KIBA KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA AMSTERDAM

Ally Kiba
Siku hizi Tanzania kumekua na mambo meeeengi yanayozushwa au kuanzia kwenye mitandao ya kijamii sanasana facebook na twitter ambapo miongoni mwa makubwa ya wiki hii ni stori kwamba mwimbaji wa Bongofleva Ally Kiba amekamatwa na polisi wa Amsterdam kwa tuhuma mbalimbali na wengine walidiriki kuripoti kwamba ni dawa za kulevya.
Ally Kiba mwenyewe aliandika kwenye page yake ya twitter kama kukanusha lakini ni tweet ambayo haikuwa rahisi kuielewa au kufahamu alichomaanisha kama unavyoona hapa chini..
Ally Kiba akanusha kukamatwa na polisi Amsterdam July 25 2013 1 
Baada ya hii tweet ilibidi millardayo.com imuendee inbox au DM kumuuliza kama ni kweli alikamatwa ambapo hili ndio jibu lake….
Ally Kiba akanusha kukamatwa na polisi Amsterdam July 25 2013 2

Huenda siku kadhaa zijazo Tanzania ikapata sheria mpya itakayokua inadili na watu wanaoitumia vibaya mitandao kama vile kutukana, kuandika uongo na mengine kama hayo… July 26 2013 Wakili Mwandamizi wa Serikali alisema makosa ya kwenye Internet yameongezeka sana Tanzania na hakuna sheria inayodili nayo moja kwa moja hivyo kuna mpango wa kuipata sheria ya hayo makosa .

3 comments:

  1. yeahp hawa watu wanaoandika habari za kutunga wachukuliwe hatua....

    ReplyDelete
  2. hatari sana kumzushia mtu uongo unamchafulia jina ,kweli kuwepo na sheria ya kubana watu wa aina hiyo

    ReplyDelete
  3. Lakini pia sio rahisi kukuzushia kitu ambacho hudeal nacho hivyo ni wakati pia wa wewe unaezushiwa kujichunguza na kuwa makini na nyendo zako maana wenda........anyway poa.

    ReplyDelete