Monday, July 01, 2013

JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA LAKANUSHA KUHUSUKIA NA VITENDO VYA UBAKAJI HUKO MTWARA


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepokea taarifa kwamba waandishi wa Habari kadhaa wamepelekwa Mtwara kwenda kumhoji msichana mmoja kwa madai ya kubakwa na wananjeshi wa JWTZ.

JWTZ  linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa endapo taarifa hizo zitatangazwa kwenye baadhi ya vyombo vya Habari wazipuuze kwani hazina ukweli  wowote zaidi  ya kuwa ni za upotoshaji.

Msichana huyo amepandikizwa ili kuharibu taswira nzuri ya JWTZ. Ifahamike kwamba maafisa na askari wa JWTZ waliopo huko Mtwara wanafanya kazi kwa uangalizi wa karibu na vitendo hivyo vya aibu hawawezi  kuvifanya. 


Jeshi letu linafanya kazi kwa nidhamu na si kama baadhi ya watu wenye maslahi binafsi wanavyolipaka matope.

Tunapenda kuwafahamisha watanzania wote kuwa JWTZ lipo kwa ajili ya maslahi ya watanzania wote.
 

Tunasikitika sana kama wapo watanzania wenye mawazo hayo machafu ya  kulichafua JWTZ lenye sifa nyingi ndani na nje ya nchi yetu.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

SLP 92023, Simu: 0764 742161

No comments:

Post a Comment