Tuesday, July 02, 2013

KWA HERI BARACK ABAMA....KARIBU TENA NA SAFARI NJEMA


Rais Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini Marekani,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini iliyoanza jana....

Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaka Kikwete,leo walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo....

Tunapenda  kuungana na  Rais Jakaya  Kikwete na  watanzania  wote  wapenda amani katika  kumshukuru Rais wa Marekani Barack Obama kwa  kuichagua  Tanzania...

Pia tunawapongeza  watanzania  wote kwa kuonyesha umoja  wetu na hata  kuzika itikadi zetu za kisiasa   na   hata  kupelekea  TV zaidi ya 1000 duniani na radio zaidi ya  3000 duniani  kuitazama  Tanzania...

No comments:

Post a Comment