Monday, July 01, 2013

MAANDALIZI YA KUMPOKEA OBAMA YAKAMILIKA..


Taswira mbalimbali zinazoonesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu. 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda vizuri, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki. 

Bendera zikiwa zimepangwa na kupangika katika upande wa lango kuu la Mashariki,Ikulu.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Kibao cha Barabara wa Barack Obama.

Jengo la Ikulu.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akisoma ratiba.
makundi ya wananchi wa Dar es salaam walikishangilia wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipopita kuwasalimia.

PICHA NA IKULU.

1 comment:

 1. HUU NI MTIZAMO TU WALA HAKUNA CHUKI KWA WAANDISHI WA BLOG ZA TANZANIA

  Waandishi wa blog hizi za matukio ya mjini tu nawaomba mwandike kona tofauti tofauti juu ya habari kubwa zinatokea na sio kona moja tu, mfano ujio wa Baraka Obama na ziara yake ya siku mbili nchini mwetu.

  Sisi wasomaji wenu tumewapa dhamana ya kutosha ya kuaamini kuzisoma blog zenu hivyo nanyi jitahidini kuturudishia thamani ya uaminifu huu na mwache kucopy and paste habari na picha kutoka blog nyingine kwenda kwenye hizo zenu yaani kila blog ina picha zile zile toka blog ya mwandishi mmoja,

  # Wasiwasi wangu mkubwa ni;

  1. Hamna vitendea kazi (kamera), basi fanyeni mpango wa hata picha za simu zinatosha kwani teknolojia ya simu sasa imekuwa na mlete tofauti wa habari zenu enyi waandishi na mkuze tasnia hii.

  2. Blog zenu ni za sebeleni zinasubiri issa michuzi kaandika nini nanyi kuandika?!.

  # Angalizo

  1. Kwa waandishi wenye tabia kama hii, punde mnakozitoa picha na habari hizi zilizoandikwa na wengine hazitakuwa mnaweza kuzinakili tena na mkifanikiwa tu basi jua umeondoka na lebo na kiunganishi cha chanzo cha habari hiyo kitu ambacho utakuwa unajirudisha nyuma kitaaluma yako hiyo ulioianzia njia panda miezi kadhaa iliyopita tu.

  2. Wadhamini mlionao punde watakukimbieni na kwenda kutangaza huko mnakozitoa habari na picha,nina wasiwasi huenda wamekwisha jitoa au hawata tangaza kabisa kwenye blog zenu..

  ReplyDelete