Tuesday, July 16, 2013

ODAMA AWAJIBU WANAOMTUHUMU KUZIFANYIA " PHOTOSHOP " PICHA ZAKE NA KUDANGANYA ALIKUWA ULAYABaada ya kuzagaa kwa habari zikimtumu mwanadada wa filamu Tanzania Jennifer Kyaka aka Odama kwamba huzifanyia makeke yaphotoshop picha zake na kuwadanganya wananchi kuwa amezipigia Ulaya, ameongea na na  mwandishi wetu  kukanusha huku akionesha picha halisi zinazomuonesha akiwa mbele.
  

Baada ya tuhuma hizo kumkabili Odama, Mwandishi wetu alimtafuta mwanadada huyo wa filamu na ndipo alipokanusha tuhuma hizo na kusema hakufanya kitu kama hicho na kwamba waliosema hivyo wanania mbaya naye.


Ili kukata ‘ngebe’ za manisnitch hao Odama ametutumia  picha hizi za ushahidi kwamba alikuwa nje ya nchi kama alivyosema.


“Kuna watu wanakosa vya  kufanya ndio maana wanakaa na kuanza kuzusha vitu ambavyo hawana uhakika navyo so siwashangai kwakuwa binadamu tunatofautiana upeo,”Odama
 
 

No comments:

Post a Comment