Monday, July 15, 2013

PRAN KRISHAN GWIJI LA FILAMU INDIA AFARIKI AKIWA NA MIAKA 93

VETERANI wa filamu Nchini India, Pran Krishan Sikand, maarufu kama Pran, amefariki dunia katika hospitali ya Lilavati jijini Mumbai Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 93 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Pran ambaye amedumu katika sanaa hii ya uigizaji kwa zaidi ya miaka 60, alikuwa maarufu kwa kucheza sehemu ya mtu katili – adui katika filamu za Kihindi.

Kati ya miaka ya 1960 na 1980, alionekana karibu katika kila filamu kali ya Bollywood, na alishinda tuzo nyingi katika kazi yake ikiwamo kubwa na maarufu ya Dadasaheb Phalke Award.

Pran amecheza filamu zaidi ya 350, maarufu zaidi ikiwa Zanjeer iliyotoka mwaka 1973 ambayo alipambana na mkongwe mwingine wa Bollywood, Amitabh Bachchan.
 
Katika filamu hii, Pran alibadilika kutoka ‘mtu katili’ na kuwa mtu mwema. Ma- starring wengine katika picha hiyo ni Ajit Khan ambaye sasa ni marehemu na wanamama Bindu Desai na Jaya Bachchan.

Filamu kama Madhumati (1958), Jis Desh Men Ganga Behti Hai (1960), Upkar (1967), Shaheed (1965), Aansoo Ban Gaye Phool (1969), Johny Mera Naam (1970), Victoria No. 203 (1972), Be-Imaan (1972), Zanjeer (1973), Don (1978) na Duniya (1984) ni miongoni mwa zilizomuweka katika daraja la juu.

No comments:

Post a Comment