Monday, July 01, 2013

WATANZANIA 60 WAKAMATWA AFRIKA KUSINI WAKATI WA ZIARA YA OBAMA

Watanzania 60 wamekamatwa Afrika Kusini kutokana na maandalizi yaliofanyika nchini humo ya kumpokea Rais Barack Obama wa Marekani. 
 Rais Obama aliwasili Afrika Kuisini  wiki iliyopita  kwa ziara ya siku tatu akitokea Senegal. Watu hao wamekamatwa baada ya kudaiwa kuishi kinyume cha sheria Afrika Kusini. 

Baada ya Watanzania hao kutiwa mbaroni na vyombo vya usalama wamehifadhiwa hapa nchini kusubiri  hatua za kisheria zaidi. 


Ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Sadiki Msele amesema Watanzania hao walirejeshwa nchini juzi  na kwamba hivi sasa wanasubiri sheria kuchukua mkondo wake.


“Safisha safisha kama iliofanyika jijini Dar es Salaam, pia imefanyika Afrika Kusini na kuwaathiri wafanyabiashara na watu wengine,” amesema ofisa huyo.

Leo mchana  Rais Obama na ujumbe wake anatarajiwa kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili na Jumanne ataondoka kurejea Marekani.

No comments:

Post a Comment