Tuesday, August 27, 2013

CHAZ BABA AFUNGA NDOA, ATINGA UKUMBI WA ‘TWANGA’ KUJINAFASI AKIWA PEKE YAKE


 Rehema akikubali kuolewa na Chaz.
Chaz akimvisha pete mkewe.
Wakikumbatiana baada ya kufunga ndoa.
Chaz Baba akimpigia simu bi harusi (mkewe) ili awahi misa ya ndoa yao. Bw. na Bi Deo Mutta waliokuwa wasimamizi wa Chaz Baba.
Chaz Baba (kulia) akiwa na marafiki zake.
Gari lililombeba bi harusi likiwasili kanisani.
Bi harusi, Rehema, kabla hajashuka.
Bi harausi akiwekwa sawa kuingia kanisani.
Chaz na Rehema wakielekea kanisani kufunga ndoa.
Chaz na mkewe wakifuatilia misa ya ndoa yao.
Mchungaji wa kanisa hilo akitoa somo la ndoa.
Maharusi wakiwa wamepiga magoti.
…Wakifungishwa ndoa.
Wakitoka kanisani.
Wakionyesha vyeti vyao.
RAIS wa bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel Cyprian ‘Chaz Baba’, juzikati aliua ndege wawili kwa wakati mmoja pale alipotoa burudani ya nguvu katika sherehe ya harusi yake  iliyofanyika katika ukumbi wa Mirado Hall uliopo Sinza Makaburini jijini Dar, na pia kutinga katika ukumbi wa Mango Gadern Kinondoni jijini Dar ambapo Twanga Pepeta walikuwa wakiendeleza wimbi la burudani katika ukumbi huo.
Tukio hilo la Chaz kutinga katika ukumbi wa Mango liliwashangaza wengi kwani kwa wakati ule Chaz alitakiwa kwenda kupumzika kutokana na mkewe kuonekana amechoka kwa sababu ya ujauzito wake.
“Shemeji yetu anaonekana kachoka sana lakini Chaz ndio kwanza anaonekana hana hata muda wa kwenda kulala mapema” alisema shabiki mmoja aliyekuwa ndani ya ukumbi.
Chaz Baba alifunga ndoa na Rehema Sospeter Marwa, siku ya Agosti 24, mwaka huu katika kanisa la St Peters jijini Dar es Salaam
.

2 comments:

  1. Vipi Oprah tuna weza tuka ongeya off this blog?

    ReplyDelete
  2. VIPI MBONA YULE DADA MWENYE KUJITIA HANAJUA SANA REHEMA KILUVYIA HAJAONEKANA? MAANA KATANGAZA MJI MZIMA YEYE NDIO KAFANYA HII ARUSI, MARA YEYE NDIO KAFANYA DECOR MSHAMBA HANA LOLOTE KAZI KUVAA MALACE WIG KAMA MDOLI

    ReplyDelete