Saturday, August 31, 2013

DIAMOND PLATNUM NI MWIZI...DAYANA NYANGE


Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange mwenye maskani yake mjini Morogoro,ambaye pia ni msanii pekee wa kike anafanya vizuri kutoka Morogoro.
Akiongea na team tizniz Dayna alisema “Kukweli ni nimekwazika sana  pia imeniuma,kwani sikutarajia msanii kama Diamond anaweza KUIBA  nyimbo yangu na kwenda kuifanya yeye.Unajua nilikuwa nataka nimshirikishe kwenye nyimbo yangu ambayo ilibidi nimefanya kwa Shedy Clever pale Tabata,hivyo nikarekodi demo,nikamtafuta na kumpatia ili aweze kusikia na kujua jinsi gani ataweza kuimba
Baada ya muda ya nikamtafuta tena vipi ili tufanye kabisa ile nyimbo,ndipo akaanza kusema yupo bize nisubiri lakini.Lakini nashangaa sasa hivi nakisikia tena ile nyimbo ameeimba yeye tena harafu kibaya zaidi ametumia beat ile ile  pia na mashairi yale yale.Kiukweli alichokifanya sio kitu kizuri,kwani watu wote tunatafuta maisha sasa yeye ameangalia zaidi maslahi yake.Na usiku wa jana ndio ametoka kuitambulisha rasmi video ya wimbo huo.
Nilikuwa namheshimu sana ila kwa hili nashindwa kusema kitu maana imenigusa sana,nyimbo yangu ilikuwa inaitwa my number one. Mpaka sasa bado sijajua nifanye kitu gani nipo katika kufikiri cha kufanya.
Team tizniz

2 comments:

  1. acheni kuharibu Kiswahili, Sema wimbo; kwani si mmoja zingekuwa nyingi ndo ungesema nyimbo` Mnatukera sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. hahahhaha waambie hao..! Mnaharibu kiswahili chetu mssh

      Delete