Monday, August 26, 2013

HATIMAYE FILAMU YA FOOLISH AGE YA LULU YAPEWA KIBALI RASMI CHA KUONESHWA..

Baada ya kutokea kwa utata kuhusu kukwama kwa filamu ya Foolish Age ya mwanadada Elizabeth Michael (Lulu) katika bodi ya filamu Tanzania, hatimaye filamu hiyo imepewa kibali rasmi cha kutolewa baada ya marekebisho yaliyotakiwa kufanyika katika filamu hiyo, kufanywa kwa mujibu wa maelekezo ya bodi hiyo
Filamu hii inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 30 mwezi huu, imepewa kibali cha kumi na sita (16) ikiwa na maana inaweza kuangaliwa kwa watu wanaoanzia na umri huo na kwenda mbele na sii vingnevyo.
Naye lulu ameonesha furaha yake kwa kupata kibali hicho kwa kuandika kwenye mtandao
“Shukrani zangu za dhati ziende kwa BODI YA UKAGUZI WA FILAMU....!!!kwa wale mliosikia kuwa filamu ya FOOLISH AGE imezuiwa ukweli ndo huu hapa...baada ya kufanyiwa marekebisho katika sehemu muhimu,hichi ndicho KIBALI KUTOKA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU...#6days to go....!!!GOD IZ GOOD...!!!asanteni kwa maombi yenu kwa wote mlioniombea...#love u all...#teamHLM..”

No comments:

Post a Comment