Thursday, August 29, 2013

HIVI NDIVYO MSANII HUYU WA FILAMU ALIVYONUSURIKA KIFO


Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu za Kibongo, Prisca Tadei hivi karibuni alinusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya pikipiki wakati alipokuwa akielekea ‘location’ kushuti.
Ajali hiyo ilitokea wiki iliyopita maeneo ya Mbagala, jijini Dar ambapo Prisca aliumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya pikipiki aliyokuwa amepanda kugongwa na gari ambapo alikimbizwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Akichonga na paparazi wetu, mkurugenzi wa kikundi anachofanyanacho kazi cha Kalunde Entertainment, Mariamu Athuman ‘Kalunde’ alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa msanii wake huyo mpaka sasa anapumua na anaonesha matumaini kwani ilikuwa ajali mbaya.
Baada ya habari hizi thesuperstarstz ilimtafuta msanii huyo kwa simu bila mafanikio na ndipo tulipompigia rafiki yake na kutujulisha kuwa anaendelea vizuri ila ameumia sana na anahitaji muda mwingi kupumzika.
 
Thesuperstarstz inamuombea msanii huyu apone ili andee na majukumu yake ya kila siku na tunaamini kwa uwezo wa mungu atapona.

No comments:

Post a Comment