Friday, August 30, 2013

"KAJALA NDIO KILA KITU KWANGU KWA SASA, YEYE NI ZAIDI YA MUME KWANGU"......WEMA

KASUMBA ya wanawake wengi kuwaambia mashoga zao siri zao nzito inadaiwa kumfanya msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu kufunguka kuwa, bila kuwa karibu na Kajala Masanja itakuwa ni kama kuamua kutembea mtupu.
Wema Sepetu na Kajala Masanja.
Wema alifikia hatua ya kutoa maneno hayo katikati ya wiki hii kwa kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonesha yeye, meneja wake Martin Kadinda na Kajala huku akisindikiza na ujumbe mzito uliosomeka:
“I always call my poch and I fell so naked without, I need her everywhere with me. I hope that’s how they out each other.”

Aliandika kimombo, alimaanisha nini?
Tafsiri ya maneno hayo ni kwamba, Wema anamchukulia Kajala kama pochi yake na bila yeye anajihisi yuko uchi kiasi kwamba anataka kila sehemu wawe wote.

Kajala amjibu
Baada ya Wema kutundika ujumbe huo, Kajala naye alijitutumua na kutupia maneno ya kumshukuru (Wema) huku akieleza kuwa, kama ni hivyo yeye hana la kusema.
Nimeyapenda maneno hayo, kama ni hivyo mimi sina la kusema,” aliandika Kajala kwenye mtandao huo.
Kwa nini Wema aseme hivyo?

Yawezekana Wema alimaanisha vingine lakini wachambuzi wa mambo wamekuwa na maoni yao huku wengi wakieleza kuwa, inawezekana Wema anasema hivyo kutokana na ukweli kwamba Kalaja anajua siri zake nyingi.
Unajua Wema amekuwa na marafiki wengi sana lakini inavyoonekana Kajala amemshiba sana na anajua siri zake nyingi. Wema anaposema bila Kajala itakuwa ni kama anatembea uchi anamaanisha kuwa, wakikorofishana kuna hatari ya kuanikana mambo yao nyeti.

Watu wanazusha kuwa Wema anauza ‘unga’, mara anatembea na kigogo mmoja serikalini, ukweli wa haya anaujua Kajala na ndiyo maana amemshiba ili siri zake ziendelee kuwa sirini,” alidai mmoja wa marafiki wa karibu wa Kajala aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mariam wa Kinondoni alisema: “Hawa wana siri nzito, kila mmoja anajua mambo ya ndani ya mwenzake na ndiyo maana hakuna ambaye yuko tayari kumtosa mwenzake, watazinguana lakini watarudiana.”

Kajala anasemaje?
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Kajala kuzungumzia maoni yake juu ya ujumbe huo wa Wema ambapo alisema, hana neno la kutia isipokuwa amefarijika tu kusikia anapendwa kiasi hicho.
“Kwa kweli hata kama wewe unaambiwa hivyo lazima utafurahi sana maana sikuwa najua kuwa napendwa na shosti wangu (Wema) ila hata mimi nampenda sana yaani siwezi kueleza, hayo manenomaneno ya watu hatuwezi kuyasikiliza,” alisema Kajala.

Msikie Wema
Nilichokiandika nilikimaanisha, Kajala kwa sasa siyo rafiki yangu tena ni ndugu ambaye nampenda sana kutoka moyoni mwangu na nitampenda siku zote na ndiyo maana sijisikii kuwa mbali naye,” alisema Wema.

Watadumu?
Swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza ni kama ushosti wa wawili hao utadumu kwani mara kadhaa imekuwa ikidaiwa kuwa wametibuana na baadaye kuonekana wako pamoja, mazingira yanayoashiria kuwa huenda siku moja wakazinguana moja kwa moja.
Hayo yanakuja kufuatia historia ya Wema ambaye amekuwa hadumu na marafiki zake, mfano ukiwa kwa msanii Snura Mushi (staa wa Majanga) ambaye waliwahi kuwa marafiki kupitiliza lakini baadaye wakatosana

No comments:

Post a Comment