Wednesday, August 28, 2013

MSHINDI WA BIG BROTHER AFRICA 2013 AZIPELEKA PESA ZAKE KANISANI

Miye,Kelvin na Elizabeth

Mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2009 Kelvin Chuwang Pam ambaye ni mume wa mshiriki mwingine wa BBA 2009 kutoka Tanzania Elizabeth Gupta amesema baada ya kupata ushindi kwenye shindano hilo aliamua kupeleka sehemu ya fedha hizo kanisani.
Kelvin anasema siku zote amekuwa akimuomba Mungu katika maisha yake na ndio maana akakumbuka kupeleka sehemu ya fedha hiyo kanisani kama Sadaka.

Akizungumzia kikubwa alichofanyia sehemu iliyobaki ya fedha hizo Kelvin amesema yeye na mke wake Elizabeth wamefungua mgahawa mkubwa nchini Nigeria ambao unauza vyakula mbalimbali vya KiNigeria na kiTanzania.
 Amesema wameamua kufungua mgahawa ikiwa ni sehemu ya kujiongezea kipato katika maisha yao ya kila siku.

Naye Elizabeth amesema mbali ya vitega uchumi ambavyo wamefungua nchini Nigeria kwasasa wanafikiria jinsi ya kuweka miradi mbalimbali Tanzania ikiwemo kuanzisha shindano la kusaka vipaji ambalo kwa Nigeria limefanya vizuri.

Aidha amesema akiwa nchini Nigeria anaendelea pia na shughuli mbalimbali ikiwemo kucheza filamu na nyota mbalimbali wa nchini humo.
 
Wakati huo huo Kelvin akafunguka kuwa mke wake Elizabeth ndiye mwanamke anayejua zaidi kupika kuliko wanawake wote aliowahi kutoka nao kimapenzi.

No comments:

Post a Comment