Tuesday, August 27, 2013

MSICHANA AMEJIKUTA AKIZOMEWA HUKU AKICHAPWA VIBOKO NA KUNDI LA WATU KATIKA ENEO LA NMC JIJINI ARUSHA BAADA YA KUVAA NGUO FUPIMsichana mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na   kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la soko la nmc jiji arusha kwa madai ya kuvaa nguo fupi hali iliyowalazimu wasamariawema kuingilia kati  na kutumia nguvu kubwa ili  kumwokoa na kumsitili kwa kumfunika na nguo zingine.

 Mwandishi wetu Halfani Lihundi  kutoka arusha alikuwapo katika sakata hilo na ametuma taarifa hii iliyosema,  watu walio shuhudia tukio hilo wamesema wamechukizwa na aina ya nguo alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania, ndiyo maana wameamua kumwadabisha ili kukomesha tabia hiyo.

Kwa upande wao wanawake waliyo msitili msichana huyo kwa kumpa nguo za heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani kabla ya kumkimbiza kwa gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na tabia hiyo inayowazalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo za kujisitili ili kujenga heshima katika jamii.

No comments:

Post a Comment