Thursday, August 29, 2013

MTITU ATISHIWA USALAMA WAKE

SIKU chache baada ya kutangaza kuanza kusambaza filamu, Mkurugenzi wa Five Effect ametishiwa usalama na watu wasiojulikana.

Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, Mtitu alipoingiza filamu yake ya Omega mapema Jumatatu hii, watu wanaodaiwa kuwa ni wamiliki wa kampuni ya kusambaza kazi za wasanii wamemtishia kuwa wana mpango wa kumdhuru yeye ili asiendelee na kazi hiyo.
“Wamepitisha meseji ya vitisho kupitia kwa watu wao wa karibu ambao ni marafiki zangu, wakanitonya kuwa wana mpango wa kuniangamiza ili nisiwaharibie biashara yao,” alisema Mtitu na kuongeza:
“Kimsingi mimi simuogopi mtu, baada ya hii Omega natarajia kuingiza filamu ya Nyati ambayo itatoka siku si nyingi

No comments:

Post a Comment