Friday, August 30, 2013

PATA HABARI KUHUSU MSIBA WA MOSES KOLOLA AMBAO UPO TEMEKE KATIKA KANISA LA EAGT


Kwa wale ambao bado hawajajua taratibu za msiba wa Askofu mkuu wa makanisa EAGT Moses kolola aliyefariki jana saa tano katika hosptali ya Africa madical investment(AMI)jijini Daresalam Ambapo mtumishi huyu wa mungu alianza kuugua na kupelekwa katika hoptali ya rufaa ya bugando huko jijini mwanza na hali ilipokuwa mbaya ndipo walipomuhamishia na kumpeleka katika hosptali ya APOLO huko nchini India na baadae kurudi akiwa katika hali nzuri.

Ila baadae Agost 16 hali ya Askofu Moses kolola ilibadilika tena na kuwaq mbaya na hapo ndipo walipompeleka katika hosptali ya Africa Madical Ivastment(AMI) ya jijini daresalam hadi mauti ilipomkuta.

Mwili wa Askofu huyo utaagwa katika EAGT viwanja vya temeke siku ya jumamosi na baadae utasafirishwa kuelekea mwanza kwa mazishitaarifa zaidi tutazidi kuwaletea ila kwa sasa waombolezaji wote mnatakiwa kufika temeke katika kanisa la EAGT.

Bado waandishi wa thesuperstarstz wapo eneo hilo na muda si mrefu watatuletea kila litakalojiri huko endelea kuwa nasisi.


No comments:

Post a Comment