Thursday, August 01, 2013

UWOYA NAKUJA KUWASHIKA, TV SHOW YANGU NI NOMA

uwoyair

Msanii bongomovie Irene Uwoya anakuja kwenye TV yako kwa njia nyingine tofauti na ya kiubunifu zaidi. Duniani kuna mastaa kadhaa ambao wanafanya reality show zao, lakini Irene Uwoya kupitia ukurasa wake wa Instagram ametoa news kwamba anaanzisha show yake binafsi kupitia kituo cha Clouds TV ambayo ni tofauti kabisa na show za mastaa wengine. 

uwoya

Undani kuhusu show hiyo ni kwamba kila kitu humo ndani kitahusu mambo ya nyumba. Irene na crew yake watakuwa na kazi ya kutembelea nyumba zenye hali mbaya na kuzifanyia ukarabati ili kuboresha hali ya mazingira ya kuishi ya muhusika mwenye nyumba au chumba. So, show yake itakuwa inaonyesha mwanzo nyumba ikiwa kwenye hali mbaya hadi atakapo ikamilisha na huo ukarabati. Hii picha inamuonyesha akiwa setting ku-shoot sehemu ya show hiyo.

No comments:

Post a Comment