Wednesday, September 18, 2013

AISHA BUI AKANA TAARIFA ZA YEYE KUKAMATWA NA ‘UNGA’ HUKO BRAZIL

HUKU kukiwa na madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui amekamatwa na kufungwa nchini Brazil kwa kunaswa na unga, mwanadada huyo ameibuka na kufafanua juu ya tuhuma hizo.

Akizungumzia swala hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu kutokea Brazil, Aisha alisema ameshangazwa na madai hayo wakati yeye yuko nchini humo akiwa amemfuata mchumba wake ambaye jina lake hakuwa tayari kulianika.
“Jamani hayo madai ya kwamba nimefungwa huku kwa kesi ya madawa ya kulevya mimi mwenyewe nayashangaa. Niko huku kwa mwezi wa nne sasa, nimekuja kwa mchumba wangu. Hizo taarifa za kwamba eti nimefungwa ni uzushi unaotengenezwa kwa nia ya kunichafua tu.

“Wakati naondoka Tanzania ilikuwa kimyakimya kwa kuwa nilijua kuna baadhi ya watu watazusha mambo ya kunipaka matope na ndicho walichokifanya.

“Naomba Watanzania wajue niko huru kabisa, naendelea na shughuli zangu kama kawaida. Natarajia kurudi Bongo hivi karibuni,” alisema Aisha.

No comments:

Post a Comment