Sunday, September 15, 2013

AKUTWA AMEKUFA NDANI YA CHUMBA CHA KUUZIA CHAKULA

Mwili wa marehemu Asha Rashid Hussein ulivyokutwa chumbani baada ya kifo chake.
Hamida Hassan na Gladness Mallya;
Asha Rashid Hussein mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es salaam amekutwa amekufa kwenye chumba cha biashara ya chakula.
Siku ya tukio walidai kuwa akiwa ameanza kukanda unga wa chapati, alijifungia ndani ya chumba hicho kilichokuwa na jiko la mkaa ambapo alianza kupika bila watu kufahamu kuwa ndani kulikuwa na mtu.
Mwadini Isaac, mmiliki wa duka.
Ilipofika muda wa saa nne bila kufunguliwa alifika kijana mmoja ambaye huwa anafanya naye kazi na kushangaa kuona hapajafunguliwa alipojaribu kufungua, aligundua kuwa mlango umefungwa kwa ndani, akaenda kumuita mama mwenye nyumba ili wafungue mlango walipofungua waligundua kuwa Asha alikuwa tayari ameshafariki na ndio wakatoa taarifa polisi Mwanananyamala ambao walifika eneo la tukio na kuamuru mwili uchukuliwe na kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi.
Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo.
Diwani wa Mwananyamala kwa Manjunju eneo lilipotokea tukio hilo, Ally Haroub alisema kuwa marehemu alikuwa akimfanyia kazi mwajiri wake,  Mwidini Isaac (picha kubwa) ambaye siku hiyo alikuwa nje ya mji lakini alipofahamishwa aliwatafuta ndugu na kuwafahamisha kilichomtokea ndugu yao.

Diwani huyo alieleza kuwa  kwa mujibu wa daktari wa Mwananyamala marehemu alifariki kutokana na kukosa hewa baada ya kuvuta gesi ya mkaa aliokuwa akipikia alipojifungia kwani ‘flame’ hiyo haikuwa na hewa kutokana na kukosa dirisha

No comments:

Post a Comment