Tuesday, September 17, 2013

BREAKING NEWS: MWANAMUZIKI HEMED MGENI MWANAMUZIKI WA ZANZIBAR NJEMA AFARIKI DUNIA

BREAKING NEWS: Mwimbaji Ahmed mgeni wa Zanzibar Njema Afariki Dunia Alfajiri ya Leo
Marehemu Ahemed mgeni enzi za uhai wake
Mwimbaji Mashuhuri wa bendi ya  Zanzibar Mjema  Ahmed Mgeni amefariki Dunia Alfajiri ya leo huko kwao Visiwani  Zanzibar alikokuwa anaugua maradhi ya muda mrefu ya  Kifua kikuu “TB”.
Mwimbaji huyo mashuhuri aliyewahi kutamba kipindi cha nyuma na bendi za Zanzibar Stars na Baadae New Zanzibar Stars na mpaka mauti yanamkuta alikuwa katika bendi ya Zanzibar Njema ambayo alikuwa anaiimbia mpaka sasa.
Mwimbaji huyo alikuwa anasumbuliwa na maradhi hayo toka akiwa Dubai baada ya hapo alirudi hapa nchini na kufikia Unguja nyumbani kwao na kulazwa katika hospital Mnazi mmoja Kisiwani humo aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupata nafuu lakini alirudishwa tena hospital baada ya hali yake kuwa mbaya mpaka mauti yamemkuta  alfajiri ya leo akiwa hospital.
Taarifa kutoka kwa familia ya marehemu zinasema mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni huko huko Unguja,Zanzibar. Mpaka mauti yanamfika marehemu Ahmedi Mgeni alikuwa bado hajaaliwa kuwa na mwenza wa maisha yake (hajaoa)
Ahmed Mgeni mpaka mauti yanamfika hii leo alikuwa ni Kiongozi wa bendi hiyo ya Zanzibar Njema Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi amina,Tunaungana na familia yake pamoja na wapenzi  muziki wa taarab nchini kwa kumpoteza mwimbaji huyo mashuhuri wa muziki wa taarab.
Moja ya nyimbo ambazo marehemu amefanya wakati wa uhai wake na ilitamba sana ni  wimbo wa Sitetereki.

No comments:

Post a Comment