Monday, September 16, 2013

HAYA NDIYO MANENO ALIYOSEMA MSANII DR CHENI BAADA YA KUTEULIWA KUWA BALOZI WA KAMPUNI MPYA YA SIMU

dr4
Wasanii wengi wa Tanzania moja ya kilio chao kikubwa ni kupata mikataba na makampuni tofauti kwa ajili ya kuwa mabalozi wa kuzitangaza bidhaa hizo.Hivi sasa mkongwe kutoka thamthilia hadi hivi sasa filamu, Dr Cheni ameteuliwa kuwa balozi wa simu mpya za kisasa ambazo zimeanza kuingia nchini aina ya Pantech.

Dr Cheni akiongea na millardayo.com amesema haya kuhusu ubalozi wake na hiyo simu,”Simu inaitwa Pantech, ni simu mpya kabisa na ina operating system ya Android version mpya. Ukizingatia sasa hivi internet ndiyo kila kitu kwenye simu za mkononi, Pantech inatumia 4G na LTE kwenye connection ya internet. Kitu kingine kizuri ni kwamba simu hii inauwezo wa kujichaji na nguvu za jua. Sasa jua letu hatutalichukia tena na pia ina camera nzuri ambayo inaitwa Spy camera yenye uwezo wa kupiga picha mbali sana.”
Dr Cheni aliendelea kuongelea kuhusu mkataba wake na majukumu yake,”Majukumu yangu hasa ni kuhakikisha simu hii watu wanatambua uwepo wake. Matangazo na promotion zinapofanyika nitakuwa na shiriki kikamilifu kabisa. Wamenipa mkataba wa mwaka mmoja kwa sasa na swali lako la thamani ya mkataba wangu naomba niweke kapuni kwasasa, ila millardayo.com itakuwa ya kwanza kujua thamani yake muda wa kuweka wazi ukifika. Ninachoweza kukwambia hivi sasa ni bei tu ya simu hizi ambayo ni Tsh 250,000 tu.”
Diamond,JB,AY,Mwana F.A,B12,Steve Nyerere ni Mzee Majuto  baadhi ya watu maarufu wa Tanzania ambao wanafanya kazi na kampuni tofauti kwa ajili ya kutangaza bidhaa zao.
dr1
dr2
dr3

No comments:

Post a Comment