Wednesday, September 04, 2013

INGRID SEPTEMBER MSANII WA KIKE ANAYE SUMBUA KATIKA TASNIA YA MUZIKI NCHINI BURUNDI

 Ingrid September  ni mmoja kati ya wasanii wa kike wanaosumbua katika tasnia ya Muziki nchini Burundi. Baada ya kuwa Video Queen wa nyimbo za wasanii kadhaa na kuonekana kuwa kivutio kwa wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini Burundi, hatimaye alijikita pia katika kuimba na kutowa Track kadhaa ambazo zimefanya vizuri.

 Msanii Ingrid September ambaye pia kijana wake ni msanii wa tasnia ya Muziki kwa sasa anajipanga kuhakikisha kwamba anafaanikisha Ndoto yake ya kuona maisha yake yanapiga hatuwa kupitia muziki. 

Katika kufikia hatua hiyo, Ingrid September amekuwa akishirikiana na wasanii wengine katika tasnia hii ya Muziki nchini Burundi, lakini pia wasanii wa tasnia ya filamu katika kuendeleza juhudi za kufikia kwenye mafaanikio.

No comments:

Post a Comment