 |
Wema Sepetu |
Muigizaji maarufu Swahiliwood Jacob Stephen(JB) amewatahadharisha mastaa
wenye majina makubwa katika tasnia ya filamu nchini kuwa wakaze buti
baada ya kuanza kupotea kisanii licha ya kuwa na majina makubwa ambapo
kwasasa chipukizi kadhaa wanaibuka na kufanya vizuri kuliko wao. JB
aliwataja wazi wazi baadhi ya mastaa wa kike kama vile Wema Sepetu,
Irene Uwoya, Aunt Ezekiel na Blandina Chagula(Johari) ambao amesema
wameanza kupotea kwenye fani tofauti na mwanzoni huku wengine wakibaki
na majina yao tu lakini hawana filamu zozote sokoni kwa muda mrefu. JB
aliyazungumza hayo hivi karibuni katika kipindi cha Take One
kinachorushwa Clouds Tv. "mimi nimewataja na siogopi, kwani hawa dada
zetu wamepotea na kubaki na majina yao tu, nawaomba kama wanataka kutoka
kwasasa waendane na mazingira ya sasa" alisema JB

JB alisema kuwa wasanii hao wamekalia kuvaa nguo fupi tu huku
wakishindwa kubadilika kutokana na wakati ambapo chipukizi wengi
wanaonekana kuwa wabunifu na kuwapita licha ya ukongwe wao. Aliongeza
kwa kusema kuwa wakati wasanii hao wanaanza kuigiza katika filamu yeye
alianza kuigiza kama baba wa lakini kwasasa anafanya vizuri katika sanaa
sababu ya juhudi zake kubwa ambazo zimemfikisha alipo sasa.
"mimi kusema kweli kila filamu nilikuwa naigiza kama baba, lakini nikawa
najifikiria nitaigiza kama baba mpaka lini, lakini nikajichanganya na
nimetoka" alisema star huyo wa filamu za Shikamoo Mzee na Nakwenda Kwa
Mwanangu.
JB
No comments:
Post a Comment