Monday, September 09, 2013

JOHN MNYIKA"NDUNGAI ALITUMWA NA NEC KUHAKIKISHA MATAKWA YA CCM YANATIMIA BUNGENI"

Mh Mnyika ktk kipindi cha "tuongee asubuhi" ndani ya startv ameeleza kuwa naibu spika mh ndugai aliagizwa na NEC kihakikisha matakwa ya ccm yanapita ktk katiba, hvyo alichokua anafanya bungeni juzi ni kutekeleza maagizo.

Pia kasema askari walioingia kuleta fujo bungeni waliandaliwa kabisa na wengine hata si askari wa pale bungeni na ana ushahidi akitakiwa kuutoa maana anawafahamu kwa sura na majina (akimaanisha ilipangwa mapema liwalo na liwe lkn matakwa ya wapangaji yatimie.

Amezungumza mengi machache ya hayo ni kuonyesha jinsi gani Zanzibar hawajashirikishwa (na yeyote anaesema wameshirikishwa na mwongo), upinzani walichokuwa wanakifanya ni "filibustering".

Pia akamalizia kwa kusema hatua inayofuata ni kurudi kwa wananchi wao ndio waamue muafaka wa katiba mpya "nguvu ya umma"

No comments:

Post a Comment