Sunday, September 15, 2013

KUFURU:J-MARTINS AMZAWADIA OMMY DIMPOZ ZAWADI YA MILION 17

Ukikutana na Ommy Dimpoz amevaa mkufu mkubwa wenye muonekano wa weusi na almasi, tambua kuwa amevaa dola 10,000 sawa na shilingi milioni 17 shingoni.
20130914-050155-600x400Ommy akiwa amevaa mkufu aliozawadia na J-Martins (Picha: Gongamx)
Mkufu huo alizawadiwa jana na staa wa Nigeria J-Martins kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa jana iliyoendana sambamba na party ya East Meets West iliyofanyika Elements Lounge.
J-Martins, Ommy Dimpoz na Man WalterJ-Martins, Ommy Dimpoz na Man Walter
“Kiukweli mimi mwenyewe nilifarijika sana,” Ommy ameiambia Bongo5.
“Niliona jamaa hatukuishia kwenye kufanya kazi lakini tumefanya kazi for the love, tumeongea vitu vingi kuhusu mipango yetu ya video. Kikubwa zaidi nilifurahi sana, bado furaha yangu ipo naona imekuwa ni kitu kikubwa kwangu, nafikiri wiki hii imekuwa wiki nzuri sana,” ameongeza.
Meneja wa Heineken Tanzanua , Uche Unigwe, Ommy, Salama na rafiki
“Ni mkufu ambao una vitu vya kung’aang’aa, kwa msanii mkubwa kama yeye kunua mkufu wa dola elfu 10 anaweza kuafford.”
DSC_6399 (900x604) (604x405)
Kuhusiana na show yake ya kesho Jumapili iliyopewa jina Tupogo Night, itakayofanyika Club Billicanas, Ommy Dimpoz amesema watu wategemee surprise pia na show kali.

No comments:

Post a Comment