Sunday, September 15, 2013

MAINDA AWAKAANGA WAUZA SURA ASEMA MUDA WAO UMEKWISHA

Mainda akiwa katika pozi
Akipiga stori na thesuperstarstz mainda alisema kuwa  kwasasa kwake wanaume sio dili sana kwani ameokoka na yupo na yesu kwahiyo hana haja na wanaume kwani amegundua wanaume ni waongo sana na hawana mapenzi ya kweli 
Msanii huyo mkali haswa anapofika mbele ya camera ameendelea kumwaga utamu kuwa hivi karibuni anategemea kuzindua kampuni yake ya filamu ambayo anauhakika itafanya poa sana kwani lengo la kampuni yake sio yeye kucheza movie kama ilivyo kwa makampuni mengine la hasha yeye kwake yupo tiyari asicheze ila mwenye kipaji na atakaendana na stori ndio atacheza filamu za kampuni yake japo n yeye atakuwa anacheza pale stori na casting maneger atakapomtaka kucheza.
Amesema kuwa kwasasa hali ya filamu zetu sio mbaya zinakuwa japo waliokuwa mastar wakubwa wameanza kuporomoka huku akiweka wazi mbele ya thesuperstarstz kuwa umefika ule wakati wawa tanzania  kujua utofauti wa pumba na mchele maana kipindi cha wauza  sura kimekwisha  na ndio maana wakongwe wanarudi kuinusuru sanaa yetu kwani mashabiki  wanataka sanaa ya kweli na sio kuuza sura .
 
Muandishi wetu alipotaka kujua wauza sura ni akina nani mainda hakuwa tayari kuwataja japo alisisitiza kuwa muuza sura sio lazima awe misss hata msichana wa kawaida ambae amevamia fani na hajui kuigiza ila anabebwa na kigezo cha uzuri wake ni muuza sura tu huku akitolea mfano kwa iren uwoya wema sepetu,Aunt Ezekiel ambao walikuwa ni mamisss ila wanafanya poa katika game kwa sababu wanajua wanachokifanya ila wale ambao wapo tu kwaajili ya kusaka waume hawa ndio jamii imewachoka na sasa wamewekwa kapuni ndio maana huwasikii tena.

Mwanadada huyo ameweka wazi kuwa wapo pia wanaume wauza sura hivyo amewaasa kufanya kazi na sio masihara kwani kwasasa wabongo wakisema hawakutaki utauzia movie zako chumbani hivyo kuweni makini alisema mainda.
Kama utakuwa na kumbukumbu mdau ni hivi karibuni vyombo  vyetu vya habari vilimkariri JB ama bonge la bwana akisema kuwa wema,uwoya,aunt johari wamepotea katika game kwa kauli hiyo inamaanisha tasnia ya filamu imeanza kujipanga kwa ajili ya kuwapembua makapi wanaoichafua tasnia.

Mnaneno kama haya pia yaliwahi kusemwa na Raisi wa shirikisho hilo la filamu tanzania bwana Saimoni Mwakifwamba kuwa atahakikisha wavaa vimini hawaigizi filamu za bongo kwani wanaiteketeza tasnia yetu.

2 comments:

  1. sibora uvaekimin lakini unakipaji sasa utamuweka anayevaa magauni marefu na hana kipaji itakuwaje sasa hehehehe mnakazi tena sio ndogo

    ReplyDelete
  2. kwanza wema na irene wana mambo mengine wanafanya ndio mana sio lazima ugande kwenye fan moja wanasaka mahela kama wema anaofice yake so yupo busy sio lazima acheze film acheni longolongo kwanza lile likingozi lao silipendi lione kwanza ovyoooooo

    ReplyDelete