Tuesday, September 10, 2013

MSANII WA FILAMU NA MUSIC BONGO SABBY ANGEL AMEFUNGA NDOA YA SIRI ANGALIA PICHA

Msanii wa filamu nchini anayekuja kwa kasi katika anga za muziki na filamu ajulikanae kwa jina la Sabby Angle ambae makazi yake ni nchini uingereza amefunga ndoa ya siri na mchumba wake wa siku nyingi thesuperstarstz inakushushia data kamili.
Wakizungumza na thesuperstarstz kwa nyakati tofauti baadhi ya wasanii bao hawakutaka kuandikwa majina yao walimuambia muandishi wa habari hizi kuwa wamesikitishwa na msanii mwenzao kuwa mchoyo kwa kufanya harusi yake kimya kimya bila kuwapa taarifa huku wakieleza kuwa hizo ni dalili za uchoyo.Msanii huyo amefunga ndowa iliyohudhuriwa na masta wachache sana na ameolewa na jamaa aliyejulikana kwa jina la Dr. Mohamed raiya wa uingereza pia
Kama utakuwa hujamjua msanii huyu amecheza katika movie ya ray inayojulikana kwa jina la Hard Price pia katika filamu ya Dk Cheni inaitwa Nimekubali Kuolewa Baada ya habari hizi kufika katika dawati letu la thesuperstarstz kwa siri tulimtafuta Sabby Angle kwa simu kutaka kujua ambapo alianza kwa salamu na kusema ...Salaam.yeah nimeshaolewa.. Na Dr.Mohamed Osman. Kutoka england. Harusi ilikuwa tareh 1. September na kwasasa Tuko hapa..ila nina mpango wa kwenda UK baada mda mchache...
Muandishi wa thesuperstarstz alimuuliza pia kutaka kujua idadi ya filamu alizocheza hadi sasa ambapo msanii huyo mkali awapo mbele ya camera alizitaja kwa kusema kwa sasa nimeshacheza
Hard Price. ya kampuni ya Rj chini ya ray na johari.. Na Coincidence.. Na Nimekubali kuolewa...ya Mahsen Awadh Dk cheni
Na  hivi karibuni naanza kucheza kwenye filamu ya Hunters ya Bond ambaye alichukua Director bora wa filamu ZFF

No comments:

Post a Comment